4 Septemba 2012 - 19:30

Kiongozi wa zamani wa masuala ya habari katika serikali ya Gadafi leo amekabidhiwa kwa serikali mpya ya Libya

televisheni ya BBC imetangaza kuwa: serikali ya Mortania imekabidhi kiongozi wa zamani wa masuala ya habari na mawasiliano wa utawala wa zamani wa Gadafi (Abdallah Sanusi) kwa serikali mpya ya Libya.Suala hilo limetokea baada ya hapo mwanzo serikali ya mortania kukataa  kumkabidhi kiongozi huyo kwa serikali ya Libya na kutaka ahukumiwe nchini humo.BBC iliongeza kusema: Sanusiy atahukumiwa kwa makosa mengi alioyafanya katika zama za utawala wake ambapo alikuwa msaidizi mkubwa wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Gadafi, sanusiy alikamatwa 17/3/2012 nchini Mortania na toka kipindi hicho mpaka sasa yalikuwa yafanyika mazungumzo kuhusu makabidhiano ya kiongozi huyo.Miongoni mwa maswali ambayo Sanusiy anatakiwa kujibu ni masuala mengi sana ikiwemo Suala la Imam Musa Sadri ambaye baada ya kufika nchini Libya katika zama za gadafi mpaka sasa hazijaja patikana taarifa zake